Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Selemani Mkomi amesema hayo leo tarehe 20 Oktoba, 2025 alipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la Kampasi ya Tanga eneo la Kange, Jijini Tanga.
Baada ya kutembelea miradi na kupata taarifa ya Utekelezaji wa Miradi huo, Katibu Mkomi amesema ameridhishwa na viwango na Utekelezaji wa Miradi huku akielekeza kuwa ni muhimu mradi kuzingatia viwango na kukamilika kwa wakati kulingana na mkataba ili kuboresha miundombinu ya utoaji huduma kwa Chuo. Pia ameeleza kuwa, serikali itaendelea kutoa fedha kuhakikisha mradi unakamilika kama ilivyotarajiwa.
Akitoa taarifa ya Mradi kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Ernest Mabonesho amesema kuwa, Mradi wa ujenzi wa Kampasi ya Tanga unahusisha ujenzi wa jengo la taaluma lenye madarasa 26 yenye uwezo kwa kuchukua wanachuo 2,500 kwa mkupuo mmoja Pamoja na ofisi 24 za watumishi.
Mradi wa ujenzi wa Kampasi ya Tanga unatekelezwa kwa awamu, ambapo kwa awamu ya kwanza ya Mradi una gharama ya kiasi cha shilingi Bilioni 6.4.
Mradi unajengwa na mkandarasi Malamla Enterprises Limited ya Jijini Dar es Salaam chini ya unasimamiwa na Mshauri Elekezi Watumishi Housing.

