Imewekwa: 11 Jun, 2026

Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kinawatangazia watumishi wote wa umma wanaotarajia kufanya Mitihani ya Utumishi wa Umma mwezi Septemba 2026 kwamba kozi ya mapitio ya mitihani itatolewa kwa njia mbili, kama ifuatavyo:

  1. Mapitio kwa njia ya ana kwa ana (Physical Classes) yatafanyika kuanzia tarehe 31 Agosti hadi 17 Septemba 2026.
  2. Mapitio kwa njia ya mtandao (Online Classes) yatafanyika kuanzia tarehe 27 Julai hadi 11 Septemba 2026.

Baada ya kukamilika kwa mapitio hayo, Mitihani ya Utumishi wa Umma itafanyika kuanzia tarehe 21 hadi 25 Septemba 2026 katika vituo vya Dar es Salaam, Dodoma, Tabora, Singida, Tanga, Mbeya na Mtwara.

Watumishi wote wanaokusudia kushiriki katika mitihani hiyo wanahimizwa kujiandikisha na kushiriki kikamilifu katika kozi za mapitio ili kuongeza uelewa na kujiandaa vyema kwa mitihani husika.

Karibu Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa maandalizi bora ya mafanikio yako katika Utumishi wa Umma

 

BONYEZA VIUNGANISHI HAPA CHINI KWA TAARIFA ZAIDI

Jisajili kwa Mafunzo ya Mapitio kwa Njia ya Mtandao

Pakua Fomu ya Maombi ya Mafunzo ya Mapitio kwa Njia ya Ana kwa Ana

Pata Maelezo Zaidi

Pakua Ratiba ya Mitihani

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo