
Taasisi ya Uongozi ya Chandler- Singapore ( CIG) kwa kushirikiana na Chama cha Utawala wa Umma na Uongozi Barani Afrika (African Association for Public Administration & Management – AAPAM) chini ya mwenyeji Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), wanaendesha Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa viongozi wa sekta ya umma barani Afrika, ijulikanayo kama “The Strong Nations for Africa Programme”. Mafunzo haya yanafanyika kwa muda wa siku tano, kuanzia tarehe 4 hadi 8 Agosti 2025, katika Ukumbi wa Palace Hotel, Jijini Arusha.
Mafunzo yamefunguliwa leo, tarehe 4 Agosti, 2025, na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais- Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bi. Mansoura Mossi Kasim. Katika hotuba ya ufunguzi, Katibu Mkuu amepongenze Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa kuwa mwenyeji wa Mafunzo haya na kuwashukuru Chama cha Utawala wa Umma na Uongozi Barani (AAPAM) na Taasisi ya Uongozi ya Chandler (CIG) kwa kuendendesha mafunzo hayo.
Katibu Mkuu amesisitiza kuwa msingi wa taifa imara siyo tu nguvu ya kiuchumi pekee, bali ni pamoja uongozi bora, uadilifu katika utumishi wa umma na imani kati ya serikali na wananchi. Hivyo, Bi. Kasim amewaeleza umuhimu wa uongozi wenye maadili na unaomjali binadamu katika kukabiliana na changamoto za uongozi na mabadiliko makubwa ya dunia.
Akiongea kabla ya mgeni rasmi, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Ernest Mabonesho, amesisitiza kuwa, pamoja na mafunzo yanayotolewa, programu hii ni wito kwa serikali na watumishi wa umma barani Afrika kuzingatia kwa dhati masuala ya uadilifu na ubunifu katika kuleta mabadiliko yenye maana katika nchi zao. Alisisitiza umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika majadiliano, tafakuri, na mijadala ya kina, itakayoboresha mustakabali wa uongozi barani Afrika.
Lengo la programu hii ni kuwawezesha viongozi waandamizi wa sekta ya umma barani Afrika kwa kuwapa ujuzi, mbinu za ubunifu na ushirikiano za uwawezesha kuongoza mabadiliko chanya katika utawala, kuimarisha taasisi, kukuza uwajibikaji, na kuchochea ustawi wa mataifa yao.
Mafunzo yamewakutanisha viongozi takribani 30 wa sekta mbali mbali za Umma kutoka nchi 9 za kiafrika zikijumuisha; Tanzania, Zambia, South Africa, Somalia, Tunisia, Kenya, Lesotho, Uganda, na Malawi.
Katika mafunzo haya, mada mbalimbali zitawasilishwa na wataalamu wabobezi kutoka barani Afrika na Singapore, zikiwemo uelewa wa dhana ya mataifa imara, dhana ya uongozi unaozingatia mabadiliko, uwajibikaji katika sekta ya umma, ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP), usawa wa kijinsia na ushirikishwaji wa kiuchumi, mapitio Mipango ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), pamoja na maono na mikakati ya muda mrefu katika kuifikia Afrika bora ijayo.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora - Zanzibar, Bi. Mansoura Mossi Kasim akitoa hotuba ya ufunguzi leo tarehe 4 Agosti 2025, katika Ukumbi wa Palace Hotel, Jijini Arusha.
Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Ernest Mabonesho akitoa hotuba ya ukaribisho wakati wa ufunguzi wa Mafunzo leo tarehe 4 Agosti 2025, katika Ukumbi wa Palace Hotel, Jijini Arusha.
Mkuu wa Taasisi ya Uongozi ya Chandler - Singapore (CIG), Ndg. Ho Wei Jiang akitoa hotuba ya utangulizi wakati wa ufunguzi wa Mafunzo leo tarehe 4 Agosti 2025, katika Ukumbi wa Palace Hotel, Jijini Arusha.
Picha za viongozi wa sekta mbali mbali za Umma kutoka nchi 9 za Tanzania, Zambia, South Africa, Somalia, Tunisia, Kenya, Lesotho, Uganda, na Malawi wakishiriki mafunzo ya Uongozi.
Picha za viongozi wa sekta mbali mbali za Umma kutoka nchi 9 za Tanzania, Zambia, South Africa, Somalia, Tunisia, Kenya, Lesotho, Uganda, na Malawi wakishiriki mafunzo ya Uongozi.
Picha za viongozi wa sekta mbali mbali za Umma kutoka nchi 9 za Tanzania, Zambia, South Africa, Somalia, Tunisia, Kenya, Lesotho, Uganda, na Malawi wakishiriki mafunzo ya Uongozi.
Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Dkt. Ernest Mabonesho akipokea zawadi kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Utawala wa Umma na Uongozi Barani Afrika (AAPAM), Prof. George Scott kwa kutambua mchango wake wa kuwezesha kufanyika kwa program ya mafunzo ya uongozi.