Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu ameipongeza kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa kuimba nyimbo zinazobeba uzalendo zenye kusukuma maendeleo mbele kwa kutangaza mambo mema yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Sangu ameyasema hayo leo katika uzinduzi kwa albamu yenye nyimbo nyimbo 25 za kizalendo ya kwaya hiyo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam akimwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene.
Pia Mhe. Sangu ameupongeza uongozi wa TPSC kwa kuongoza na kuisimiamia vizuri kwaya hiyo ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika matukio mbalimbali yakiwemo ya Serikali.
Awali kabla ya kumkaribisha Naibu waziri Sangu kuzindua kwaya hiyo na kuongoza harambee, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa TPSC, Dkt. Ernest Mabonesho alisema kuwa, kazi kubwa ya chuo cha utumishi wa Umm ani kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma na kwaya ya chuo cha utumishi wa umma imekua chombo muhimu katika utoaji elimu kwa umma hasa kuchochea maendeleo ya nchin yetu.
Sambamba na uzinduzi, Mhe. Sangu amengoza harambee ya kuchangia kwaya hiyo na kiasi cha shilingi milioni 123 kimechangwa katika hafla hiyo.