Chuo kinatoa mafunzo ya muda mfupi na ya muda mrefu.

1.Mafunzo ya Muda mfupi

Mafunzo ya muda mfupi yanayotolewa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania yameandaliwa kuwaejengea uwezo watumishi wa umma kubadili fikra na kukuza ujuzi kwa lengo la kuongeza tija na ufanisi katika utumishi wa Umma.

Mafunzo haya yanaandaliwa kwa kuzingatia;

  • mahitaji yanayoibuliwa na chuo kupitia tathmini ya mahitaji ya mafunzo na
  • mahitaji mahsusi ya wateja.

Walengwa wa Mafunzo ya muda Mfupi ni watumishi wa umma kutoka Wizara, Wakala na Mamlaka, Idara za Serikali zinazojitegemea na serikali za mitaa.

2.Mafunzo ya muda mrefu

Mafunzo ya muda mrefu yanatolewa kwa ngazi za Astashahada ya Awali, Astashahada, Stashahada na Shahada ya kwanza yanayozingatia miongozo ya mafunzo ya NACTVET na TCU. Mafunzo haya yanawaandaa watumishi wa umma watarajiwa na sekta binafsi katika fani mbalimbali wanaokidhi vigezo vya mahitaji ya soko la ajira nchini.

Walengwa wa kozi za muda mrefu  ni wahitimu wa kidato cha nne na sita na wahitimu wa ngazi mbalimbali za elimu wenye sifa na nia ya kujiendeleza kwenye ngazi za juu za elimu katika fani zinazotolewa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania.

Ngazi za Astashahada ya Awali, Astashahada na Stashahada

  • Utawala wa umma,
  • Menejimenti ya Kumbukumbu, Nyaraka na Taarifa,
  • Mafunzo ya Uhazili,
  • Menejimenti ya Rasilimali watu na Menejimenti ya Ununuzi na Ugavi.

Ngazi ya Shahada:

  • Shahada ya Menejimenti  ya Kumbukumbu na Nyaraka
  • Shahada ya Uhazili na Utawala.

BONYEZA HAPA KUPATA MAELEZO YA KINA YA KOZI ZETU ZA MUDA MREFU

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo