Imewekwa: 20 Jun, 2025
MHE. SANGU AKIPONGEZA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA KWA UTENDAJI WA KAZI

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Clement Sangu, ametoa pongezi hizo wakati banda la Chuo cha Utumishi wa Umma leo tarehe 20 Juni 2025, katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika viwanja vya Chinangali Park, Jijini Dodoma.

Akizungumza katika banda la chuo, Mhe. Sangu amesema anaridhishwa  na mafanikio makubwa yaliyofikiwa na chuo katika utekelezaji wa majukumu yake. Amepongeza maandalizi mazuri ya ushiriki wa chuo katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma   na huduma zinazotolewa na chuo, hasa uanzishwaji wa mafunzo ya mitihani ya watumishi wa umma (PSE Review Courses) yanayofanyika kwa njia ya mtandao. Amesema kuwa mfumo huu wa kidigitali unawawezesha watumishi wa umma kushiriki mafunzo hayo popote walipo, hivyo kuokoa gharama na muda, na kuwapa fursa ya kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi

 

Aidha, Naibu Waziri amezitaja huduma zinazotolewa na chuo kwa watumishi na wananchi kuwa ni za kiwango cha juu, zikiwa na lengo la kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma kwa ujumla. Pia, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kukiwezesha chuo cha utumishi wa Umma kuboresha miundo mbinu ili kuboresha huduma zinazotolewa.

Ameongeza kuwa, chuo kinatoa mchango mkubwa katika kuimarisha utumishi wa umma nchini kwa kutoa mafunzo na ushauri wa kitaalamu unaoendana na mahitaji ya sasa. Hii inachangia kuleta mabadiliko chanya katika utendaji wa watumishi wa umma na kuboresha huduma kwa wananchi kwa ujumla.

Kwa kuhitimisha, Mhe. Sangu pia amekipongeza chuo kwa kuandaa na kuendesha kongamano la kwanza la Utumishi wa Umma kwa mafanikio makubwa. Kongamano hili, ambalo lilitekelezwa kwa ushirikiano kati ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) na Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar (IPA), liliandaliwa kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya utumishi wa umma, likilenga kuimarisha ushirikiano kati ya viongozi, teknolojia, na ubunifu ili kuleta mabadiliko chanya katika sekta hii muhimu.

Mhe. Sangu alipata maelezo ya kina kuhusu huduma zinazotolewa na chuo katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma  kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Bw. Shakiru Abdulkarim kwa niaba ya Mkuu wa chuo na Mtendaji Mkuu.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Clement Sangu, akiweka saini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Chuo cha Utumishi wa Umma katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika viwanja vya Chinangali Park, Jijini Dodoma, leo tarehe 20 Juni 2025.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Clement Sangu, akitoa pongezi kwa chuo cha utumishi wa umma baada ya kutembelea banda la Chuo cha Utumishi wa Umma leo tarehe 20 Juni 2025, wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika viwanja vya Chinangali Park, Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus Clement Sangu, akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko, Bw. Shakiru Abdulkarim, kwa niaba ya Mtendaji Mkuu, alipotembelea banda la Chuo cha Utumishi wa Umma leo tarehe 20 Juni 2025, wakati wa Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika viwanja vya Chinangali Park, Jijini Dodoma.

 

 

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo