Uendelezaji Stadi,Maarifa na Utambuzi katika Menejimenti , Uongozi, Utawala na Usaidizi wa Ofisi. Haya yatafikiwa kwa kutoa Programu za Mafunzo bora, zinazotokana na mahitaji na hali halisi.
- Kutoa huduma za ushauri katika Menejimenti ya Utumishi wa Umma
- Kuwa na uwezo wa kutoa mafunzo (wingi, aina na ubora) yanayokidhi mahitaji ya Utumishi wa Umma
- Kusambaza maarifa kuhusu Menejimenti bora ya Utumishi wa Umma (mwenendo bora), hii itafikiwa kwa kufanya utafiti tumizi na uchapishaji wa matokeo ya utafiti huo.
- Kutoa Diploma na Vyeti kwa wahitimu waliofaulu katika programme za kitaaluma na kuboresha CSTC na TSC (Zamani) kuwa Taasisi ya Mafunzo ya Utumishi wa Umma yenye ufanisi na inayokidhi mahitaji ya Utumishi wa Umma.Hii itafanikiwa kwa kiasi fulani kwa kuingia katika ushirikiano wa kimkakati na Taasisi za mafunzo na maendeleo za umma na za binafsi na watu mmoja mmoja.
Chuo kitazingatia zaidi programu zake kwenye “kuboresha utendaji” ingawa pia kitatoa programu chache za kitaaluma zilizokusudiwa kuwaanda waliomaliza shule kwa ajira bora katika Utumishi wa Umma kama njia nyingine ya ajira kwenye sekta binafsi.Programu za kitaaluma zitasaidia kupata sifa zinazotambuliwa rasmi au zilizothitishwa na zitajumuisha program za kiwango cha Diploma na Cheti.
Kulingana na mamlaka, kazi na malengo, TPSC inatakiwa kutoa mafunzo jumuishi na yanayohusiana na programu za maendeleo kwenye ngazi zote za utumishi wa umma (kama vile ngazi ya chini na ya kati).
TPSC inatoa masomo ya Shahada ya kwanza katika Uhazili na Kumbukumbu, Nyaraka na Usimamizi wa Taarifa kuanzia Septemba, 2017 kwenye Kampasi ya Dar es Salaam.