Imewekwa: 19 Jul, 2025
TPSC YAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA CHUO - KAMPASI YA SINGIDA

Singida, 18 Julai, 2025

Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kimeendelea kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia kwa kutekeleza  miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TPSC, Dkt. Florens M. Turuka, pamoja na Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu, Dkt. Ernest Mabonesho, walihudhuria makabidhiano ya ujenzi wa Kampasi ya Singida awamu ya pili yaliyofanyika  eneo la Mungu Maji, Manispaa ya Singida tarehe 18 Julai,2025.

 Utekelezaji wa mradi ulianza rasmi tarehe 7 Oktoba, 2023, kwa utaratibu wa Nguvu Kazi (Force Account), ukiwa chini ya usimamizi wa mtaalamu mshauri kutoka Arusha Technical College kwa gharama ya ujenzi huu ni Shilingi Bilioni 1.3 kwa mapato ya ndani.

Mradi huu  ulihusisha ujenzi wa majengo manne yenye vyumba nane vya madarasa. Vyumba viwili kati ya hivyo vina uwezo wa kuchukua wanachuo 480 kwa wakati mmoja, huku vyumba vingine viwili vikiwa na uwezo wa kubeba wanachuo 240 kwa wakati mmoja. Aidha, majengo haya yanajumuisha ofisi 12 za walimu na wafanyakazi, vyumba vya mikutano, vyoo, pamoja na vyumba vinne maalum kwa watu wenye mahitaji maalum.

 

Kukamilika kwa mradi huu ni sehemu ya mkakati wa chuo wa kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia, ukiwa ni mpango wa kuhakikisha wanachuo wanaendelea kupata mazingira bora zaidi ya kujifunzia na kufundishwa. Lengo ni kuimarisha ubora wa huduma zinazotolewa na chuo, pamoja na kuhakikisha wanachuo wanapata mazingira yanayowezesha mafanikio kitaaluma.

Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu, Dkt. Ernest Mabonesho (wa pili kutoka kushoto), na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TPSC, Dkt. Florens M. Turuka (wa kwanza kushoto), wakipokea funguo za majengo ya Kampasi ya Singida kutoka kwa Arch. Richard, mtaalamu mshauri kutoka Arusha Technical College, wakati wa hafla ya makabidhiano ya majengo hayo eneo la Mungu Maji, Singida, tarehe 18 Julai 2025.

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo