Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania anapenda kuwatangazia wahitimu wote na wadau wa Chuo kuwa, Mahafali ya arobaini na Mbili (42) ya Chuo cha Utumishi wa Umma kwa Kampasi zote yanatarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa, tarehe 28 Novemba, 2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNICC), Dar es Salaam kuanzia saa tatu (03.00) Asubuhi.
Aidha, wahitimu wote wanahimizwa kuhudhuria mazoezi (Rehearsal) yatakayofanyika siku ya Alhamisi tarehe 27 Novemba 2025 katika Kampasi ya Dar es Salaam kuanzia saa nane (08.00) mchana. Wahitimu wanatakiwa kuvaa Joho na suti ya rangi nyeusi au dark blue.
Wahitimu wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kupitia namba. 0679031848/0629820870.
ORODHA YA WAHITIMU
Limetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano na Masoko

