Dira
Kuwa kituo cha ubora katika kuchochea ujifunzaji na ubunifu ili kutoa huduma bora kwa umma
Dhima
Kujenga uwezo na ujuzi wa sekta ya umma kupitia mafunzo, tafiti tumizi, shauri za kitaalamu na majukwaa ya kiteknolojia ya ushirikishanaji ili kuboresha utoaji wa huduma kwa umma
Maadili Yetu
Kuthamini Mteja: Tutatoa huduma bora ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wadau.
Uadilifu: Tunazingatia viwango vya juu zaidi vya kimaadili, uaminifu na kuzingatia Utawala Bora katika kutekeleza majukumu.
Weledi: Tunazingatia kiwango cha juu cha umahili na viwango bora katika kutekeleza majukumu ili kukidhi mahitaji na matarajio ya wadau.
Ubunifu: Tunadumisha ubunifu endelevu katika matumizi ya technolojia zinazofaa ili kukuza na kutoa huduma bora.
Ushirikiano katika Kazi: Tunajenga na kuhimiza uhusiano wa kikaziwa kirafiki na shirikishi miongoni mwawatumishi katika kufikia malengo ya kitaasisi.
Kutoa Huduma bila upendeleo: Tunazingatia usawa na kuepuka ubaguzi wa aina yoyote ya upendeleo katika utoaji wa huduma.

