Imewekwa: 25 May, 2025
DKT. MABONESHO ASISITIZA UTOAJI HUDUMA BORA NA USHIRIKIANO KWA WATUMISHI WA KAMPASI YA MTWARA.

Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho amesema hayo katika kikao na watumishi wa Kampasi ya Mtwara wakati wa ziara ya kukagua utendaji kazi wa kampasi hiyo. Katika kikao hicho, alisisitiza umuhimu wa utoaji wa huduma bora kwa wateja, ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wanachuo kwa upendo na kuwapa miongozo ili waweze kufikia malengo yao kitaaluma.  “Utoaji wa huduma bora ni miongoni mwa misingi ya Maaadili ya Chuo cha Utumishi wa Umma” alisema Dkt. Mabonesho. 

Aidha, Dkt. Mabonesho aliwapongeza watumishi wa Kampasi ya Mtwara kuendelea kuchapa kazi kwa bidii  na  kuwahimiza  kudumisha ushirikiano miongoni mwao  ili kuongeza tija na kufanikisha malengo  ya chuo kwa pamoja. Katika kikao hicho, watumishi walipata fursa ya kutoa maoni yao  na kuelezea changamoto zinazokumba utendaji wa kazi na huduma zinazotolewa kwa wanachuo.

Kwa upande wa watumishi wa Kampasi ya Mtwara wakiongozwa na Mkurugenzi wa KampasiBi. Juslina Tuzza, walimpongeza Mkuu wa Chuo na Menejimenti ya chuo kwa kwa juhudi za kuendelea kuboresha miundo mbinu ya kujifunzia na kufundishia, pamoja na kujali stahiki za watumishi.

Kabla ya kikao na watumishi, Dkt. Mabonesho alipata fursa ya kutembelea miundo mbinu ya kujifunzia na kufundishia katika kampasi hiyo, ili kuona maendeleo na changamoto. Pia Mkuu wa Chuo alipata fursa ya kuongea na serikali wa wanachuo pampoja na baadhi ya wanachuo. Katika ziara hiyo ya kiutendaji, Mkuu wa chuo alimabatana na Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia masuala ya kitaaluma, utafiti na maendeleo, Dkt. Hamisi Amani.

Mkuu wa Chuo na Afisa Mtendaji Mkuu, Dkt. Ernest Mabonesho akiongea na Watumishi wa Kampasi ya Mtwara  alipotembelea kampasi hiyo tarehe 22  Mei, 2025

Baadhi ya Watumishi wa Kampasi ya Mtwara wakimsikiliza Mkuu wa Chuo na Afisa Mtendaji Mkuu, Dkt. Ernest Mabonesho katika mkutano uliofanyika tarehe 22 Mei, 2025.

 

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo