Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kinapenda kuwataarifu waombaji wote kuwa orodha ya waombaji waliochaguliwa kujiunga na Kozi za Shahada katika Kampasi za Dar es Salaam na Tabora awamu ya kwanza imewekwa hapa chini;
- Waliochaguliwa Shahada ya Kwanza – Kampasi ya Dar es Salaam
- Waliochaguliwa Shahada ya Kwanza – Kampasi ya Tabora
Waombaji waliochaguliwa kujiunga na TPSC lakini pia wana nafasi za udahili katika taasisi nyingine wanatakiwa KUTHIBITISHA udahili wao kwa TPSC ili kuhifadhi nafasi yao.
🔐 Utaratibu wa Uthibitisho
Tafadhali fuata hatua zifuatazo ili kukamilisha uthibitisho wa udahili:
- Ingia kwenye Mfumo wa Maombi Mtandaoni (OAS) 👉 [oas.tpsc.go.tz]
- Ingia kwenye akaunti yako kwa kutumia jina la mtumiaji (username) na nenosiri (password).
- Ingiza KODI YA (MASIMBO WA) UTHIBITISHO iliyo/uliotumwa kwenye simu yako kupitia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kutoka TCU.
- Endapo hukupokea au umepoteza kodi hiyo, unaweza kuomba itumwe tena kwa kubofya kiungo cha “Request Confirmation Code” kilichopo chini ya kisanduku cha kuingiza kodi ya uthibitisho.
- Baada ya kuthibitisha, mfumo utakupatia moja kwa moja:
- Barua yako ya Udahili
- Maelekezo ya Kujiunga (Joining Instructions)
📞 Msaada wa Kiufundi
Kwa msaada wa kiufundi, tafadhali wasiliana na kampasi husika kupitia namba za simu zilizoonyeshwa kwenye Mfumo wa Maombi Mtandaoni (OAS).
TPSC inawapongeza waombaji wote waliochaguliwa na inatarajia kuwakaribisha katika jamii ya ubora na weledi katika utumishi wa umma.

