Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho, anapenda kuwatangazia wahitimu wote na wadau wa Chuo kuwa, Mahafali ya arobaini na tatu (43) ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kwa Kampasi zote yatafanyika siku ya Jumamosi, tarehe 13 Juni 2026 katika Viwanja vya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Kampasi ya Mtwara, kuanzia saa tatu (03:00) Asubuhi. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Ridhiwani Jakaya Kikwete.
Wahitimu wote wanahimizwa kuhudhuria mazoezi (rehearsal) yatakayofanyika siku ya Ijumaa, tarehe 12 Juni 2026 katika Kampasi ya Mtwara kuanzia saa nane (08:00) mchana. Wahitimu wanatakiwa kuvaa joho na suti ya rangi nyeusi au buluu iliyokolea (dark blue).
Wahitimu wote wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kupitia namba: 0756 264 567 / 0737 326 474.
ORODHA YA WAHITIMU

