Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), anawatangazia wahitimu wa kidato cha Nne na cha Sita, kujiunga na Chuo Cha Utumishi wa Umma kwa mafunzo ya muda mrefu kwa ngazi ya Astashahada(CHETI) na Stashahada (DIPLOMA) kwa Mwaka wa Masomo 2026/2027 katika Kampasi za Dar es Salaam, Tabora, Mtwara, Tanga, Singida na Mbeya kwa kozi zifuatazo:
- Menejimenti ya Kumbukumbu, Nyaraka na Taarifa
- Mafunzo ya Uhazili na Utawala
- Menejimenti ya Rasilimali Watu
- Utawala wa Umma
- Ununuzi na Ugavi
SIFA YA KUJIUNGA:
CHETI: Mwombaji awe amemaliza Kidato cha Nne na awe amefaulu angalau masomo Manne (4) (yasiyokuwa ya dini) kwa kiwango cha kuanzia alama D, Au Cheti cha kidato cha nne pamoja na Cheti cha VETA (NVA level III)
DIPLOMA: Mwombaji awe na Cheti cha awali (NTA level 4) kutoka Chuo chochote kinacho tambulika na NACTVET, AU Cheti cha kumaliza Kidato Cha Sita (6) chenye Principal Pass Moja na Subsidiary Moja au Zaidi.
Dirisha la kwanza la udahili litakuwa wazi kuanzia 28 Mei hadi 1o Julai 2026
Kwa taarifa zaidi tafadhali tembelea tovuti cha Chuo www.tpsc.go.tz au wasiliana nasi kwa namba zifuatazo;
Kampasi ya Tabora: 0794234594/0737326481
Kampasi ya Dar es Salaam: 0794123495/0737326472
Kampasi ya Tanga: 0794123402/0737326488
Kampasi ya Singida: 0748764566/0737326477
Kampasi ya Mbeya: 0745234575/0737326479
Kampasi ya Mtwara: 0756 264 567 / 0737 326 474

