Mitihani ya Utumishi wa Umma kwa watumishi wa umma ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu cha (I) cha Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma. Pia Sheria ya Utumishi wa Umma namba 8 ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2008 ilitoa mamlaka kwa Chuo cha Utumishi wa Umma kuendesha hiyo tangu mwaka 2003.

Mitihani ya utumishi wa Umma hufanyika mara mbili kwa mwaka (Februari na Agosti) kwa muda wa wiki nne. Wiki tatu za kwanza ni za  darasa la mapitio (review  classes) na wiki moja ya mwisho ni kwa ajili ya watumishi kufanya mitihani yenyewe.

Kada zinazohusika na mitihani ya utumishi wa umma na programu za mapitio ni pamoja na:

  • Usimamizi wa Nyaraka kwa Wasaidizi wa Kumbukumbu  (Higher Standard Records Management)
  • Mtihani wa Waendeshaji Simu (Telephone Operators);
  • Maendeleo ya Usimamizi kwa Wasaidizi wa Watendaji Wakuu I;
  • Maendeleo ya Usimamizi kwa Wasaidizi wa Watendaji Wakuu II;
  • Mtihani wa Umahiri kwa Maafisa Rasilimali Watu;
  • Mtihani wa Umahiri kwa Maafisa Kumbukumbu;
  • Mtihani wa Umahiri kwa Maafisa Ustawi wa Jamii
  • Mtihani wa Umahiri kwa Maafisa Kazi;
  • Sheria kwa Maafisa Tawala;
  • Sheria kwa Maafisa Watendaji wa Kata/Tarafa; na
  • Mtihani wa umahiri kwa Maafisa Maendeleo ya vijana;

 

MITIHANI YA WATUMISHI WA UMMA - SEPTEMB, 2026

 

Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kinawatangazia watumishi wote wa umma wanaotarajia kufanya Mitihani ya Utumishi wa Umma mwezi Septemba 2026 kwamba kozi ya mapitio ya mitihani itatolewa kwa njia mbili, kama ifuatavyo:

  1. Mapitio kwa njia ya ana kwa ana (Physical Classes) yatafanyika kuanzia tarehe 31 Agosti hadi 17 Septemba 2026.
  2. Mapitio kwa njia ya mtandao (Online Classes) yatafanyika kuanzia tarehe 27 Julai hadi 11 Septemba 2026.

Baada ya kukamilika kwa mapitio hayo, Mitihani ya Utumishi wa Umma itafanyika kuanzia tarehe 21 hadi 25 Septemba 2026 katika vituo vya Dar es Salaam, Dodoma, Tabora, Singida, Tanga, Mbeya na Mtwara.

Watumishi wote wanaokusudia kushiriki katika mitihani hiyo wanahimizwa kujiandikisha na kushiriki kikamilifu katika kozi za mapitio ili kuongeza uelewa na kujiandaa vyema kwa mitihani husika.

Karibu Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kwa maandalizi bora ya mafanikio yako katika Utumishi wa Umma

 

BONYEZA VIUNGANISHI HAPA CHINI KWA TAARIFA ZAIDI

Jisajili kwa Mafunzo ya Mapitio kwa Njia ya Mtandao

Pakua Fomu ya Maombi ya Mafunzo ya Mapitio kwa Njia ya Ana kwa Ana

Pata Maelezo Zaidi

Pakua Ratiba ya Mitihani

 

 

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo