Imewekwa: 09 Nov, 2026

Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania anapenda kuwatangazia wahitimu wote na wadau wa Chuo kuwa, Mahafali ya arobaini na nne (44) ya Chuo cha Utumishi wa Umma kwa Kampasi zote yanatarajiwa kufanyika   siku ya Jumatatu, tarehe 7 Desemba, 2026 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam kuanzia saa tatu (03.00) Asubuhi.

Aidha, wahitimu wote wanahimizwa kuhudhuria mazoezi (Rehearsal) yatakayofanyika siku ya Jumapili tarehe 6 Desemba 2026 katika Kampasi ya Dar es Salaam kuanzia saa nane (08.00) mchana. Wahitimu wanatakiwa kuvaa Joho na suti ya rangi nyeusi au dark blue.

Wahitimu wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kupitia namba. 0794123495/0737326472

Limetolewa na

Kitengo cha Mawasiliano na Masoko

 

ORODHA YA WAHITIMU

KAMPASI YA DAR ES SALAAM

KAMPASI YA TABORA

KAMPASI YA MTWARA

KAMPASI YA MBEYA

KAMPASI YA TANGA

KAMPASI YA SINGIDA

 

 

 

 

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo