Imewekwa: 09 May, 2025
DK. MABONESHO AKUTANA NA WATUMISHI WA KAMPASI YA DSM: AHIMIZA WATUMISHI  KUFANYA KAZI KWA BIDII NA KUTOA HUDUMA BORA.

Mei 9,  2025  

Mkuu wa Chuo na Afisa Mtendaji Mkuu, Dkt. Ernest Mabonesho, alifanya ziara rasmi katika Kampasi ya Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha huduma na utendaji kazi wa kampasi. Ziara hii ilikuwa na malengo makuu ya kuzungumza na watumishi wa kampasi na kujua changamoto zinazowakumba katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Katika mkutano huo, Dkt. Mabonesho aliwasihi watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kuzingatia sheria, taratibu, na kanuni za utumishi wa umma ili kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa wateja wa chuo zinakuwa bora zaidi. Aidha, alitoa wito kwa watumishi kuendeleza maadili mema ya utumishi na kuimarisha nidhamu kazini ili kuleta tija katika utendaji wao wa kila siku.

Kwa upande wa Watumishi wa Kampasi ya Dar es Salaam, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kampasi hiyo, Musa Lugembe, walitoa shukrani za dhati kwa Mkuu wa Chuo kwa jitihada zake za kuendelea kuboresha mazingira ya kazi, miundombinu ya kampasi na kujali maslahi ya watumishi.  Pia, walimshukuru kwa juhudi za kukamilisha ujenzi wa Kampasi ya Singida, jambo ambalo linaongeza fursa kutoa huduma.

Pia, watumishi walimshukuru Mkuu wa Chuo kwa juhudi zake za kukamilisha ujenzi wa Kampasi ya Singida na kuanza ujenzi wa Kampasi Tanga, jambo ambalo litapanua wigo wa  utoaji wa huduma bora katika chuo.

Katika kuonyesha dhamira ya kuendelea kuboresha utendaji kazi wa kampasi hiyo, Mkuu wa Chuo alikabidhi rasmi gari jipya kwa Mkurugenzi wa Kampasi ya Dar es Salaam. Gari hili linatarajiwa kuwa chachu ya kuimarisha usafiri na ufanisi wa utendaji kazi wa kampasi, na kuleta tija zaidi katika utoaji wa huduma.

Katika ziara hiyo, Mkuu wa Chuo alimbatana na Makamu Mkuu wa Chuo -Taaluma, Tafiti na Shauri za Kitaalam Dkt. Hamis Amani Nalinga na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo -Mipango, Fedha na UtawalaDkt. Charles T. Rwekaza

Mkuu wa Chuo na Afisa Mtendaji Mkuu, Dkt. Ernest Mabonesho akiongea na Watumishi wa Kampasi ya Dar es Salaam alipotembelea kampasi hiyo tarehe 9 Mei, 2025

Baadhi ya Watumishi wa Kampasi ya Dar es salaam wakimsikiliza Mkuu wa Chuo na Afisa Mtendaji Mkuu, Dkt. Ernest Mabonesho katika mkutano uliofanyika tarehe 9 Mei, 2025.

 

Mkuu wa Chuo na Afisa Mtendaji Mkuu, Dkt. Ernest Mabonesho akimkabidhi gari Mkurugenzi wa Kampasi ya Dar es Salaam, Bw. Musa Lugembe kwa ajili ya kuboresha utendaji wa Kampasi hiyo.

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo