Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, anawatangazia wahitimu wa kidato cha nne na cha sita, kujiunga na Chuo Cha Utumishi wa Umma kwa mafunzo ya muda mrefu kwa ngazi ya Astashahada(CHETI) na Stashahada (DIPLOMA) kwa Mwaka wa Masomo 2025/2026 katika Kampasi za Dar es Salaam, Tabora, Mtwara, Tanga, Singida na Mbeya kwa kozi zifuatazo:
- Menejimenti ya Kumbukumbu, Nyaraka na Taarifa (Records, Archives and Information Management)
- Mafunzo ya Uhazili na Utawala (Secretarial Studies and Administration)
- Menejimenti ya Rasilimali Watu (Human Resource Management)
- Utawala wa Umma (Public Administration)
- Ununuzi na Ugavi (Procurement and Supply Management)
SIFA YA KUJIUNGA:
CHETI: Mwombaji awe amemaliza KIDATO CHA NNE na awe amefaulu angalau masomo MANNE (4) (yasiyokuwa ya dini) kwa kiwango cha kuanzia alama D, Au Cheti cha kidato cha nne pamoja na Cheti cha VETA (NVA level III)
DIPLOMA: Mwombaji awe na Cheti cha awali (NTA level 4) kutoka Chuo chochote kinacho tambulika na NACTVET, AU Cheti cha kumaliza KIDATO CHA SITA (6) chenye PRINCIPAL PASS MOJA na SUBSIDIARY MOJA au Zaidi.
Kwa taarifa zaidi au msaada kuhusu maombi ya kujiunga na Chuo, wasiliana nasi na Kampasi zetu kwa namba zifuatazo:
- Kampasi ya Tabora:0744647403
- Kampasi ya Dar es Salaam: 0713577587
- Kampasi ya Tanga: 0718410687
- Kampasi ya Singida: 0719646383
- Kampasi ya Mbeya: 0784321301
- Kampasi ya Mtwara: 0712129977