Imewekwa: 06 May, 2025
Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), kinawatangazia watumishi wote wa Umma wanaotarajia kufanya mitihani ya Utumishi wa Umma kwa mwezi Agosti, 2025 kuwa kozi ya mapitio ya mitihani itafanyika kuanzia tarehe 4 hadi 22 Agosti, 2025 kwa watahiniwa watakaohudhuria kwa njia ya ana kwa ana na kwa upande wa mapitio kwa njia ya mtandao yataanza tarehe 8 Julai hadi 15 Agosti, 2025 na kufuatiwa na mitihani itakayofanyika kuanzia arehe 25 hadi 29 Agosti, 2025 katika vituo vyote vya Dar es Salaam, Tabora, Mtwara, Singida, Tanga, Mbeya na Dodoma.