Uongozi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania unawatangazia wanachuo wote waliohitimu masomo yao katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, kuhakiki taarifa zao za Usajili na Mitihani katika mfumo wa NACTVET ili wajiridhishe kama taariza zao ziko sahihi.
Moja ya faida za taarifa kuwa sahihi kwenye mfumo wa NACTVET ni kumuezesha mwanachuo husika kupata namba ya utambulisho (AVN) inayotolewa na NACTVET pindi atakapohitaji kujiendeleza kwa masomo ya elimu ya juu zaidi.
Uhakiki unaweza kufanyika kupitia kiunganishi (link) cha Students’ information verification) kinachopatikana kwenye anwani hii:
https://nactvet.go.tz/index.php/student-information-verification
au, tembelea tovuti ya NACTVET (https://nactvet.go.tz/ ) na fungua menyu ya “Students’ Information verification”.
Kila mwanachuo ajihakiki kujiridhisha na mambo yafuatayo;
- Kwamba YUPO kwenye mfumo wa NACTVET na katika mfumo huo anaonekana katika mwaka na muhula sahihi kulingana na hatua ya masomo aliyofikia katika mafunzo yake chuoni;
- Kwamba matokeo yake hadi muhula wa mwisho yanaonekana kuwa yamewasilishwa NACTVET.
Endapo mwanachuo atabaini mapungufu yoyote katika taarifa zake, awasiliane na ofisi ya Usajili au Mitihani kwa namba zifuatazo;
Kampasi |
Usajili |
Mitihani |
Meneja Taaluma |
Dar es Salaam |
0752989383 |
0713577587 |
0754620129 |
Tabora |
0764775034 |
0717152111/ 0717574525 |
0757837882 |
Mtwara |
0712624005 |
0712129977 |
0652331919 |
Singida |
0785211644 |
0719646383 |
0745221050 |
Tanga |
0688205484 |
0746731101 |
0766919618 |
Mbeya |
0769571122 |
0784321301 |
0754832382 |