Kampasi ya Tabora

Kampasi ya Tabora kwa Ufupi

Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Kampasi ya Tabora kilichokuwa kikijulikana kwa jina la Chuo cha Uhazili Tabora ni Kampasi ya pili ya zamani baada ya Kampasi ya Dar es Salaam kilichokuwa kikijulikana kama Chuo cha Mafunzo ya Utumishi wa Serikali. Chuo cha Uhazili Tabora kilianzishwa ili kujaza pengo la upungufu wa watumishi wa Ofisini na hasa Wahazili baada ya kupata Uhuru Tanzania. Ujenzi wa Chuo ulianza Septemba 1970 na kukamilika na kuanza kufanya kazi Oktoba, 1973. Chuo hiki kimekuwa na mabweni manne ya wanafunzi 600, wanaume 300 na wanawake 300 na maeneo ya michezo na burudani.

Mwaka 2000 Chuo cha Uhazili Tabora na Chuo cha Mafunzo cha Utumishi wa Serikali viliunda Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kwa Sheria ya Wakala za Serikali Na. ya 2000.

Wakati wa kuanzishwa kwake ilikuwa na mihula miwili ya wiki 21 kwa mwaka, hasa kutilia mkazo Mafunzo ya awali na Mafunzo tarajali ya Uhazili na wakufunzi 29 tu. Hivi sasa Kampasi hii ina zaidi ya kozi 5, na wakufunzi wa kudumu 23 na wa muda 21 na Zaidi ya wanafunzi 2563 wanachukua program za Cheti na Diploma.

Tuko wapi?

Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania Kampasi ya Tabora kipo Mtaa wa Itetemya, Kata ya Kanyenye Manispaa ya Tabora mkabala na Makao makuu ya  Polisi mkoa wa Tabora.

 



Kampasi inatoa  mafunzo ya muda mrefu kwa ngazi ya Astashahada (Cheti) na  Stashahada (Diploma) katika kozi zifuatazo;-

  1. Uhazili (NTAL Level 4 to NTA Level 6)
  2. Utunzaji Kumbukumbu, Nyaraka, na Taarifa (NTAL Level 4 to NTA Level 6)
  3. Menejimenti ya Rasilimali Watu (NTAL Level 4 to NTA Level 6)

Huduma za Malazi

-----

Huduma za Afya

-----

Dawati la Jinsia

-----

Ushauri Nasaha

-----

Serikali ya Wanafunzi

-----

Madarasa

----

Maabara za Upigaji Chapa

----

Maabara za Kompyuta

----

Maktaba

-----

 

 

Mkurugenzi wa Kampasi

Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania

S.L.P 329

Tabora

Simu: +255 26 260 5387

Nukusi: +255 26 260 45 37

Barua Pepe: tabora@tpsc.go.tz

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo