Kampasi ya Singida ni miongoni mwa Kampasi sita za Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania. Kampasi ya Singida ilianzishwa rasmi Mwezi wa Saba (7) mwaka 2011 ikiwa ni kampasi ya nne kuanzishwa kati ya Kampasi sita za Chuo. Kuanzishwa kwa Kampasi ya Singida ni utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa aliyekuwa Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda tarehe 23 Novemba, 2009 wakati akifungua kampasi ya Mtwara. Kamapasi ya Singida ipo Barabara ya Uwanja wa Ndege, Kata ya Mandewa -Manispaa ya Singida.
Kampasi ya Singida ipo Barabara ya Uwanja wa Ndege, Kata ya Mandewa -Manispaa ya Singida. Kampasi ya Singida inatoa kozi mbalimbali kuanzia ngazi ya astashahada na stashahada. Miongoni mwa kozi hizo ni pamoja na astashahada ya utunzaji wa kumbukumbu, astashahada ya uhazili, astashahada ya menejimenti ya rasilimaliwatu na astashahada ya utawala wa umma (NTA,4) pamoja na stashahada ya utunzaji wa kumbukumbu, stashahada ya uhazili, stashahada ya menejimenti ya rasilimaliwatu na stashahada ya utawala wa umma (NTA 5& 6). Aidha, Kampasi ya Singida ni kituo cha mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi wa umma, shauri za kitaalamu na ni kituo cha mafunzo na mitihani kwa watumishi wa umma
Ili kuwasaidia wanachuo kupata ujuzi kwa lengo la kukuza weledi wao na maendeleo ya taaluma zao katika fani mbalimbali walizochagua , kampasi ya Singida ipo katika mazingira mazuri ambayo yana-:
Kampasi ya Singida inatoa huduma zake za kitaaluma kupitia kwenye madarasa ya kisasa na yanayopitisha hewa ya kutosha, maabara za kisasa za kuchapia, maabara za kisasa za komputa, maktaba nzuri yenye vitabu vya kisasa, mtandao wa kutosha kuwezesha wanachuo kujitafutia mahitaji yao ya kujifunzia kwenye vyanzo mbalimbali, n.k. Aidha, Kampasi ina watumishi ( Walimu na Wasiowalimu) wanaojituma, wenye weledi, hamasa na wenye vipaji vya kutosha kufanya kazi ya kuwajengea uwezo wanachuo katika Nyanja tofauti tofauti kwa utiifu na uaminifu mkubwa.
Mkurugenzi wa Kampasi
Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania
S.L.P 1534
Singida
Simu: +255 26 2502933/3082
Nukushi +255 26 250 3082
Barua Pepe: singida@tpsc.go.tz
Mrejesho, Malalamiko au Wazo