Imewekwa: 24 Oct, 2024
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAIPONGEZA OFISI YA RAIS UTUMISHI NA TAASISI ZAKE KWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE KIKAMILIFU

 Na. Veronica Mwafisi-Dodoma

Tarehe 21 Oktoba, 2024

 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na taasisi zake kwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuhakikisha huduma bora inatolewa kwa wananchi kwa wakati sahihi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama ametoa pongezi hizo leo jijini Dodoma kwa niaba ya kamati yake wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

“Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imesheheni wabobezi wa sekta zote jambo linalowafanya watendaji wa ofisi hii pamoja na taasisi zilizopo chini yake kutekeleza majukumu yake kikamilifu.” Mhe. Dkt. Mhagama amesema.

Aidha Dkt. Mhagama ameishukuru Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa kamati hiyo kwani wajumbe wake wamekuwa wakipatiwa uelewa mpana juu ya utekelezaji wa majukumu ya kila taasisi.

Katika hatua nyingine, Mhe. Dkt. Mhagama ameishauri Ofisi ya Rais- UTUMISHI na Utawala Bora kutoa mrejesho mara kwa mara kwa wananchi juu ya hatua mbalimbali ambazo imekuwa ikizichukua na kuzifanyia kazi baada ya kupokea malalamiko au changamoto ya masuala mbalimbali ili kuonesha namna ambavyo ofisi hiyo imekuwa ikiwajibika na kutekeleza majukumu yake kwa kiwango kikubwa.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria itapokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kwa siku mbili, tarehe 21 na 22 Oktoba, 2024.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imemaliza kikao kazi chake cha siku mbili kwa kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora pamoja na baadhi ya taasisi zake ikiwemo  Chuo cha Utumishi wa Umma( TPSC),TASAF, eGA na Taasisi ya UONGOZI.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Joseph Mhagama akiongoza kikao kazi cha kamati yake na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakiwa katika kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo kwa mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akitoa ufafanuzi wa moja ya hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Deus Sangu akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024 kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene.

Katibu Mkuu-IKULU, Bw. Mululi Majula Mahendeka akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi wa ofisi hiyo kwa mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi akitoa ufafanuzi wa hoja iliyowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Ernest Mabonesho akitoa ufafanuzi wa hoja za masuala ya mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho zilizowasilishwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa kikao kazi cha kamati hiyo na Watendaji wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na taasisi zake kilicholenga kupokea na kujadili taarifa ya utendaji kazi ya mwezi Aprili hadi Septemba 2024.

 

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo