Wananchi wote mnatangaziwa kwamba, Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kitaondosha mali chakavu kwa njia ya mnada wa hadhara vikiwemo vifaa vya TEHAMA, SAMANI na vifaa chakavu mchanganyiko mbalimbali katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Tabora, Singida na Mbeya katika tarehe na vituo kama inavyoonekana hapa chini.
Na |
Tarehe ya Mnada |
Aina ya Mali |
Mali Zilipo |
1 |
17 Septemba, 2024 |
Vifaa chakavu mbalimbali |
Ofisi za Chuo, MAKAO MAKUU DAR ES SALAAM – Mtaa wa Barabara ya Bibi Titi Mohamed (Kituo A) |
2 |
17 Septemba, 2024 |
Vifaa chakavu mbalimbali |
Ofisi za Chuo, KAMPASI YA DAR ES SALAAM-Mtaa wa Magogoni -Tarehe (Kituo B) |
3 |
17 Septemba, 2024 |
Vifaa chakavu mbalimbali |
Ofisi za Chuo, KITUO CHA MAFUNZO KWA NJIA YA MTANDAO-DAR ES SALAAM-Jengo la IFM, Block A, Mtaa wa Shaaban Robert - (Kituo C) |
4 |
17 Septemba, 2024 |
Vifaa chakavu mbalimbali |
Ofisi za Chuo, KAMPASI YA TABORA– Mtaa wa Itetemya (Kanyenye) |
5 |
17 Septemba, 2024 |
Vifaa chakavu mbalimbali |
Ofisi za Chuo, KAMPASI YA SINGIDA-Mtaa wa Utumishi |
6 |
17 Septemba, 2024 |
Vifaa chakavu mbalimbali |
Ofisi za Chuo, KAMPASI YA MTWARA-Mtaa wa Shangani |
7 |
17 Septemba, 2024 |
Vifaa chakavu mbalimbali |
Ofisi za Chuo, KAMPASI YA MBEYA-Mtaa wa Sokomatola |
8 |
17 Septemba, 2024 |
Vifaa chakavu mbalimbali |
Ofisi za Chuo, KAMPASI YA TANGA-Mtaa wa Kange. |
MASHARTI YA MNADA
- Kifaa kitauzwa kama kilivyo na mahali kilipo (as is where is basis);
- Mtu yeyote atakaye tamka bei ya juu kisha akashindwa kulipa asilimia mia moja (100%) ya bei aliyotamka, atachukuliwa kuwa ni mwenye kutaka kuvuruga mnada na hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
- Mnunuzi atalipia asilimia mia moja (100%) ya thamani ya kifaa/vifaa atakavyonunua na kuchukua/kuondoa kifaa/vifaa atakavyonunua siku ya mnada;
- Ruhusa ya kuangalia mali zinazokusudiwa kuuzwa itatolewa ndani ya siku mbili (2) kabla ya tarehe ya mnada husika;
- Mnada utaanza saa nne (04:00) kamili asubuhi katika kila kituo kwa mtiririko uliooneshwa; Kwa vituo vyenye vituo vidogo yaani A,B na C, mnada utaanza kituo A na kufuatia B na kisha kituo C.
- Wananchi wote mnakaribishwa kushiriki katika mnada huu wa hadhara.
IMETOLEWA NA
AFISA MTENDAJI MKUU NA MKUU WA CHUO
CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA TANZANIA