Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, anapenda kuwatangazia wahitimu wa kidato cha nne na cha sita, kujiunga kwenye mafunzo ya muda mrefu kwa ngazi ya CHETI (Certificate) na STASHAHADA (Diploma) kwa Muhula wa Machi 2025 katika Kampasi za Tabora, Mtwara, Tanga, Singida na Mbeya kwa ngazi ya Diploma na Cheti kwa kozi zifuatazo:
- Utunzaji Kumbukumbu, Nyaraka na Taarifa
- Uhazili
- Usimamizi wa Rasilimali watu
- Utawala wa Umma
- Ununuzi na Ugavi
SIFA ZA KUJIUNGA:
CHETI: Mwombaji awe na Cheti cha kumaliza KIDATO CHA NNE chenye ufaulu wa angalau masomo MANNE (4) kwa kiwango cha kuanzia alama “D” bila kuhusisha masomo ya dini, Au Cheti cha Form IV pamoja na Cheti cha VETA (NVA level III).
DIPLOMA: Mwombaji awe na Cheti cha awali (NTA level 4) kutoka Chuo chochote kinacho tambulika na NACTVET, Au Cheti cha kumaliza KIDATO CHA SITA (6) chenye PRINCIPAL PASS MOJA na SUBSIDIARY MOJA au zaidi.
Tuma maombi yako kupitia Online Application System: https://oas.tpsc.go.tz BONYEZA HAPA KUTUMA MAOMBI
Dirisha la udahili litafungwa tarehe 28 Februari 2025
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba zifuatazo:
- Tabora Kampasi: 0764775034
- Tanga Kampasi: 0718410687
- Singida Kampasi: 0752151185
Mbeya Kampasi: 0784321301 - Mtwara Kampasi: 0712129977/0712129977