Imewekwa: 01 Nov, 2024
Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), kinawatangazia watumishi wote wa Umma wanaotarajia kufanya mitihani ya Utumishi wa Umma kwa awamu ya March 2025 kuwa mafunzo kabla ya mitihani yatafanyika kuanzia tarehe 17 Febuari, 2025 hadi 7 March, 2025 na kufuatiwa na mithani itakayofanyika kuanzia tarehe 10 hadi 14 March 2025. katika vituo vyote vya Dar es Salaam, Tabora, Mtwara, Singida, Tanga, Mbeya na Dodoma.