Imewekwa: 21 Oct, 2025
Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), kinawatangazia watumishi wote wa Umma wanaotarajia kufanya mitihani ya Utumishi wa Umma kwa mwezi Machi, 2026 kuwa kozi ya mapitio ya mitihani itafanyika kuanzia tarehe 9 hadi 27 Machi, 2026 kwa watahiniwa watakaohudhuria kwa njia ya ana kwa ana na kwa upande wa mapitio kwa njia ya mtandao yataanza tarehe 9 Februari hadi 20 Machi, 2026 na kufuatiwa na mitihani itakayofanyika kuanzia arehe 30 Machi hadi 3 Aprili, 2026 katika vituo vyote vya Dar es Salaam, Tabora, Mtwara, Singida, Tanga, Mbeya na Dodoma.