Imewekwa: 13 Nov, 2024

Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania anapenda kuwatangazia wahitimu wote na wadau wa Chuo kuwa, Mahafali ya arobaini (40) ya Chuo cha Utumishi wa Umma kwa Kampasi zote yanatarajiwa kufanyika   siku ya Ijumaa, tarehe 6 Desemba 2024 katika ukumbi wa Mkapa uliopo eneo la Sokomatola, jijini Mbeya kuanzia saa tatu (03.00) Asubuhi.

Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb).

Aidha, wahitimu wote wanahimizwa kuhudhuria mazoezi (Rehearsal) yatakayofanyika siku ya Alhamisi tarehe 5 Desemba 2024 katika Kampasi ya Mbeya kuanzia saa nane (08.00) mchana. Wahitimu wanatakiwa kuvaa Joho na  suti ya rangi nyeusi au dark blue. Gharama ya Joho ni shilingi 30,000 kwa wahitimu.

Wahitimu wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kupitia namba. 0769571122/0658890011/0784321301/0683532777.

Majina ya wahitimu yanapatakana kwenye tuvuti ya Chuo (www.tpsc.go.tz).

WOTE MNAKARIBISHWA

 

Limetolewa na

Kitengo cha Mawasiliano na Masoko

Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo