
Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania ( TPSC) tarehe 27 Januari 2024 kimesaini mkataba wa ujenzi na mkandarasi Malamla Enterprises Limited ya Jijini Dar es Salaam wa ujenzi wa majengo ya Kampasi ya Tanga katika eneo la Kange, Jiji la Tanga unaotarajiwa kukamilika ndani ya miezi nane.
Mkataba huo unahusisha ujenzi wa majengo ya madarasa yenye uwezo kwa kuchukua wanachuo 2,500 kwa mkupuo mmoja pamoja na ofisi. Mkataba huo wenye thamani ya Bilioni 1.7 ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa Kampasi ya Tanga ambao mpaka kukamilika utagharimu kiasi cha shingi Bililio 6.4. Mradi huo wa ujenzi unasimamiwa na Mshauri Elekezi ambaye Kampuni ya Watumishi Housing.
Akizungumza wakati wa utiaji saini, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho amesema kuwa ana uhakika kuwa mradi utakamilika ndani ya muda uliopangwa na kusisitiza mkandarasi kuhakikisha anatimiza wajibu wake kwa mujibu wa mkataba.
Hafla ya utiaji saini mkataba huo imefanyika katika Kampasi ya Tanga iliyopo pia eneo la Kange na kuhudhuriwa na watumishi wa Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Tanga, Mshauri elekezi na wadau.
Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho (kulia) akimkabidhi mkataba mkandarasi wa ujenzi wa majengo ya Kampasi ya Tanga, Bw. Malamla ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Malamla Enterprise Limited mara baada ya kusaini makubalinao hayo tarehe 27 Januari 2025.
Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumshi wa Umma Dkt. Ernest Mabonesho ( aliyesimama katikati) akishuhudia utiaji saini makubaliano ya ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma,Kampasi ya Tanga katika ya Mkurugenzi wa Kampasi ya Tanga, Bi Zawadi Rashid (wa pili kutoka kulia aliyekaa) na Mkurugenzi Mtendaji wa Malamla Enterprise Limited, Bw. Malamla ( wa pili kutoka kushoto aliyekaa) ambaye ni mkandarasi.
Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Ernest Mabonesho(wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa mkandarasi Malamla Enterprises Limited kuhusu eneo la Mradi wa Ujenzi wa Kampasi ya Tanga wakati wa kukabidhi eneo la kazi mara ya Mkataba wa kusainiwa leo tarehe 27 Januari 2025.