Imewekwa: 26 Oct, 2024
WAZIRI SIMBACHAWENE: WAAJIRIWA WAPYA WAPATIWE MAFUNZO ELEKEZI KUBORESHA UTENDAJI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene (Mb) ametoa rai kwa Chuo cha Utumishi wa Umma pamoja na waajiri kuhakikisha wanawapatia waajiriwa wapya Mafunzo Elekezi ya Awali (Induction Training) ili kuboresha utendaji kazi wao wanapoingia serikalini.

Mhe. Simbachawene ameyasema hayo katika ziara ya kikazi alipotembelea Chuo cha Utumishi wa Umma, Kampasi ya Dar es Salaam na kuongea na watumishi.

“Hakikisha waajiriwa wapya wote wa serikali wanapata mafunzo Elekezi (Induction course) ili kuwajengea misingi ya utendaji bora wanapongia serikalini” amesisitiza Mhe. Simbachawene.

Mhe Simbachawene amesema, jukumu kubwa la Chuo cha Utumishi wa Umma ni kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi wa umma yakiwemo mafunzo Elekezi hivyo, ameelekeza Chuo hicho kuendelea kuongeza ubunifu ili kuhakikisha waajiriwa wapya wanapata mafunzo elekezi.

Katika ziara hiyo, Mhe. Simbachawene akiwa na mwenyeji wake ambaye ndiye Mkuu wa chuo na Afisa Mtendaji Mkuu, Dkt. Ernest Mabonesho alipata fursa ya kukagua miundombinu ya kufundishia ya kujifunzia ya Kampasi ya Dar es Salaam.

Awali akitoa taarifa ya Utendaji kiujumla, Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma nchini, Dkt. Ernest Mabonesho amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, Kampasi ya Dar es Salaam pekee imefanikiwa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi 1, 289.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Watumishi wa Chuo cha Utumishi wa  Tanzania katika Kampasi ya Dar es Salaam wakati wa  ziara ya kikazi iliyofanyika Oktoba 25, 2024.

Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), Dkt. Ernest Mabonesho akiwasilisha Taarifa ya Utendaji ya Chuo mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, Oktoba 25, 2024.

 

Watumisi wa TPSC- Dar es Salaam, wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati wa  ziara ya kikazi iliyofanyika Oktoba 25, 2024.

 

 

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo