Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kilianzishwa mwaka 2000 kwa sheria ya Wakala za Serikali Na. 30 ya mwaka 1997. Lengo la kuanzishwa kwake lilikuwa kuziba pengo la kuwa na taasisi ya mafunzo jumuishi kwa utumishi wa umma kukidhi mahitaji yanayobadilika ya utumishi wa umma yaliyosababishwa na maboresho ya utumishi wa umma na haja ya kuwa na chuo cha utumishi wa umma kinachojitegemea chenye uwezo wa fedha endelevu.
Kutokana na hali hiyo, TPSC ni mtoa huduma ya maarifa na stadi anayependelewa kwa utumishi wa umma katika maeneo ya uongozi, Usimamizi wa Kimkakati, Utawala, maadili na uwajibika. Pia ni taasisi ya kujenga utamaduni wa elimu endelevu kwa watumishi wa umma. Wateja wa TPSC ni pamoja na Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, idara zinzojitegemea, Wakala za Serikali, wanaohitimu elimu ya Sekondari, umma kwa jumla na sekta binafsi.
TPSC ina Kampasi sita zilizojengwa kimkakati jijini Dar es Salaam, Tabora, Mtwara, Singida, Tanga na Mbeya ili iwe karibu na wateja wake nchi nzima.
Taasisi inatoa masomo katika viwango vitatu vya Cheti (Basic Technician Certificate), Diploma na Shahada ya Kwanza (BA) myanayofaa kwa sekta ya umma na binafsi katika Kampasi zake.Licha ya Programu hizo, TPSCinatoa masomo ya mapitio kwa ajili ya Mitihani ya Utumishi wa Umma na Huduma za Ushauri.Hivi karibuni imeanza ktumika mtindo wa Elimu na Mafunzo yanayotokana na Weledi. (CBET) kama njia ya maendeleo, namna ya kupata Elimu bora na Mafunzo yanayokidhi mahitaji ya soko la ajira la kudumu na linalo haraka sana.
Chuo cha utumishi wa umma Tanzania kimesanifu upya tovuti yakekwa manufaa ya wateja, wadau na umma kwa jumla. Tovuti hii ni chombo cha kupasha habari kinachokusudiakuuarifu umma kwa jumlakuhusu Chuo cha Utumishi umma, huduma inazozitoa, muundo wake na shughuli za chuo kwa jumla.
Inatarajiwa kwamba, tovuti hii iliyoboreshwa itakuwa chanzo cha taarifa kinachofaa kwa wateja wetu, wadau na umma kwa jumla.
Tunawakaribisha wote mtembelee tovuti yetu.www.tpsc.go.tz